Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Akson akitoa maelekezo wakati wa mkutano wa Bunge unalioendelea mjini Dodoma jana.
Mbunge wa
Viti Maalum Tabora mjini Mhe. Mwanne Nchemba (CCM) akichangia hoja
wakati kujadili hoja ya Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi,
Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene
na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapemajana Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge wa
Arusha mjini Mhe. Godbless Lema (CHADEMA) akichangia hoja wakati
kujadili hoja ya Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na
Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene na Angella
Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma
Wabunge
wakifuatilia mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi,
Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene
na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma
Mbunge wa
Chalinze Ridhiwani Kikwete akiongea na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji
Peter Msigwa (katikati) mara baada ya kumalizika mkutano wa Bunge jana
mjini Dodoma.(P.T)
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi Seleman Jafo akiwa katika picha
ya pamoja na wageni wake waliomtembelea jana Bungeni, mjini Dodoma.
WAZIRI wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwa katika picha ya
pamoja na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jana Bungeni,
mjini Dodoma. (Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma)
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.
Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amewapongeza
wabunge kwa kushiriki vizuri mashindano ya Muungano yaliyofanyika
Zanzibar na kurudi salama mjini Dodoma kuendelea na majukumu yao.
Pongezi
hizo za Spika zimetolewa leo Bungeni Dodoma na Naibu Spika Dkt. Tulia
Akson kwa niaba ya Spika alipokuwa akitoa matangazo kabla ha kuahirisha
shughuli za Bunge hadi jioni ambapo Bunge linaendelea kujadili hoja ya
Hotuba za Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa
na Mawaziri George Simbachakene na Angella Kairuki iliyowasilishwa
mapema leo.
Timu za
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizoshiriki mashindano hayo
ni timu za mpira wa miguu na pete ambapo timu ya mpira wa pete imefanya
vizuri kwa kuishinda timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa magoli
18 kwa magoli 15 wakati timu ya mpira wa miguu zilitoka sare ya
kufungana goli 1:1
Kushiriki
kwa Wabunge katika mashindano hayo yamelenga kuimarisha udugu uliopo
kati ya pande mbili za Muungano na kuwapa fursa Wabunge kufanya mazoezi
kwa ajili ya kujenga na kuimarisha afya zao.
Aidha,
michezo kwa Wabunge inatoa nafasi kubwa ya ushirikiano ambayo ni
kielelezo cha msingi kinachozaa Viongozi bora wanaotokana na sekta ya
michezo.
Wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wanafursa kubwa ya kufanya mazoezi
mbalimbali katika kujenga na kuimarisha timu za Bunge hilo ili kujenga
pia ujirani mwema.
Ushiriki
wa Wabunge kwenye mashindano siyo mara ya kwanza, Wabunge hao hushiriki
michezo mbalimbali, wanashiriki mpira wa miguu wakiwa watani wa Jadi wa
timu za Simba na Yanga, Februari 4, 2012 walishiriki mazoezi ya viungo
yaliyoendeshwa na klabu inayojulikana kama “Kitambi noma” kutoka mjini
Unguja kwa kuzingatia Bunge lina eneo mahususi la kufanyia mazoezi
mazoezi ya viungo (Gym).


0 comments :
Post a Comment