Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungao wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Kassim Majaliwa Majaliwa amewakaribisha wafanya biashara kutoka nchini
Singapore kuja kuwekeza nchini Tanzania kutokana na fursa zilizopo
nchini katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Waziri
Mkuu ametoa rai hiyo leo mjini Dododma alipokuwa akiongea na Ujumbe wa
Singapore ulioongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Biashara na
Viwanda Mhe. Kol Poh Koon aliyeambatana na wafanyabiashara mashuhuri
kujifunza na kujionea fursa zilizopo nchini katika masuala ya biashara
na uwekezaji.
Waziri
Mkuu Majaliwa amesema kuwa anaamini kampuni za Singapore zitakazowekeza
nchini zitakuwa na tija katika sekta ya mafuta na gesi asilia, kilimo,
Uchukuzi pamoja na Viwanda katika kuwaletea maendeleo Watanzania.
Kuhusu
kuimarika kwa ushirikiano kati Tanzania na Singapore, Waziri Mkuu
Majaliwa amesema kuwa Serikali iko mstari wa mbele katika kuhakikisha
inawajengea uwezo watumishi wake katika kada za uhandisi, sheria na
wachumi ambao watakuwa msaada mkubwa katika sekta ya mafuta na gesi
inayokua nchini ambapo Singapore wamepiga hatua kubwa katika sekta hiyo.
Kwa
upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Biashara na Viwanda kutoka
nchini Singapore Mhe. Dkt. Kol Poh Koon ameishukuru Tanzania kwa
kuendelea kushirikiana na nchi yake huku akionesha kuridhishwa kwake na
uhusianao mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Waziri
huyo wa Biashara na Viwanda kutoka nchini Singapore amesema kuwa nchi
yake itatoa ushirikiano mkubwa kwa Tanzania katika kuhakikisha
inawajengea uwezo watendaji wakuu wa Serikali ili Tanzania iweze kufikia
malengo waliojiwekea katika kuwahudumia wananchi wake.
Aidha,
awali akiongea na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.
Makame Mbarawa, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Medalled
Karemaligo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage,
Mhe. Dkt. Kol amesema kuwa nchi yake itatumia rasilimali walizonazo
ikiwemo rasilimali watu kuwafundisha wataalamu kutoka Tanzania ili waje
kuwafundisha wataalamu wengine hapa nchini kwa manufaa ya nchi hizo
mbili.
Kuhusu
Bandari ya Dar es salaam, Mhe. Dkt. Kol amesema kuwa bandari hiyo ni
nzuri ikilinganishwa na bandari nyingine zilizopo katika ukanda wa
Bahari ya Hindi kwa kuwa ipo karibu zaidi na Singapore hali ambayo
itarahisisha biashara baina ya nchi hizo mbili.
Katika
kuonesha nchi yake inavyojali ushirikiano na Tanzania, Mhe. Dkt. Kol
amemkaribisha Waziri wa Nishati na Madini kwenda kushiriki wiki ya
nishati nchini Singapore ambayo huadhimishwa Oktoba kila mwaka.
Ujumbe
huo kutoka nchini Singapore upo nchini kwa muda wa siku tano kuanzia
Aprili 26 hadi 30, 2016 ambapo wanatembelea maeneo mbalimbali ya ikwemo
Dar es salaam, Dodoma na mkoa wa Morogoro ambapo watazindua mradi wa
ushirikiano utakaojulikana kama “Star City”.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akisalimiana
na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Singapore, Dkt. Koh Poh Koon na
ujumbe wake, Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akizungumza na
Waziri wa Biashara na Viwanda wa Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia
kwake) na ujumbe wake, Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27,
2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto)
akiongea na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Singapore, Dkt. Koh Poh
Koon (katikati) leo mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Balozi wa Singapore
nchini Tanzania.







0 comments :
Post a Comment