Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. John Haule amekutana na kikosi cha cha timu ya Taifa ya soka, Taifa Stars pamoja na viongozi wa timu hiyo  pamoja na kupiga picha na kuzungumza nao huku akiwatoa hofu ya maisha na usalama wakiwa Nairobi, Kenya. 
Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani.
Anaripoti  Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas,  kutoka Kenya.
Kikosi kikifanya duaKikosi cha timu ya soka ya Tanzania-Taifa Stars, kikikifanya dua kwenye Uwanja wa Camp Toyoyo uliopo Jericho, nje kidogo ya jiji la Nairobi. Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani.
Dida goliniKipa wa timu ya soka ya Tanzania-Taifa Stars, Deogratius Munishi maarufu kwa jina la Dida, akifanya mazoezi ya kuzuia penalti kwenye Uwanja wa Camp Toyoyo uliopo Jericho, nje kidogo ya jiji la Nairobi.  Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani.
maguli na kabundaMshambuliaji Elius Maguri na Kiungo Hassan Kabunda wakipumzika katika mazoezi hayo.
Mazoezi ya viungoStars wakifanya mazoezi ya viungo
Balozi Dk. Haule akiwa na Taifa Stars nje ya hoteli ya Nairobi Safari ClubBalozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. John Haule akipiga picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya soka ya Tanzania baada ya kuzungumza nao na kuwatoa hofu ya maisha na usalama wakiwa Nairobi, Kenya. Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani. (Picha zote na Alfred Lucas wa TFF).