Michezo
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) imemalizika hapo jana na Simba SC
ikijikuta ikiangukia nafasi ya tatu baada ya kupokea kichapo cha goli
2-1 kutoka kwa JKT Ruvu na hivyo kusalia na alama 62 huku Azam
wakifikisha alama 64 na kushika nafasi ya pili baada ya kutoa sare ya
goli 1-1 na Mgambo JKT, shabiki wa damu wa Simba, Mohammed Dewji ‘MO’
ameamua kufunguka yaliyo moyoni mwake kutokana na matokeo hayo.
Mara
baada ya kumalizika kwa mchezo wa Simba na JKT Ruvu, MO ambaye pia ni
Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises
Tanzania Limited (METL Group) alitoa yaliyo moyoni kwake kuhusu Simb
kupitia ukurasa wake wa Twitter, ujumbe ambao ulionekana kuwagusa
mashabiki wa Simba na wadau wengine wa michezo nchini.
MO aliandika “#Simba mnatunyima raha, tumechoka kutaniwa na kutukanwa mitaani”
Aidha mashabiki wa Simba na wadau wa michezo nchini hawakuwa nyuma kutoa na wao maoni yao kuhusu mwendendo wa Simba.
Wakati
MO akiandika hayo, Mwana FA ambaye naye ni shabiki wa Simba SC
aliandika ujumbe ambao ulionekana kuwa na maumivu na kuwatumia ujumbe
viongozi wa klabu hiyo.
Blogger Comment
Facebook Comment