Rais
mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete alimtabiria Rais John Magufuli
kuwa atapunguza kiwango cha Kodi ya Mshahara (PAYE) kutoka tarakimu
mbili hadi kufikia moja.
Jumapili
akiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yaliyofanyika
kitaifa mkoani Dodoma, Rais Magufuli alitangaza kupunguza kodi ya
mshahara kutoka asilimia 11 hadi 9.
Punguzo
hilo la PAYE ambalo litaanza kutumika katika mwaka huu wa fedha unaonza
Julai mosi, lilitabiriwa na Kikwete, mwaka jana katika maadhimisho ya
siku kama hiyo.
Katika hotuba yake, Kikwete alisema kodi ya mshahara imekuwa ikipunguzwa mwaka hadi mwaka katika kipindi cha uongozi wake.
“Tumeendelea kupunguza kiwango cha kodi ya mapato kwa wafanyakazi mwaka hadi mwaka.
“Tulikuta
kodi ikiwa asilimia 18.5. Sasa imefikia asilimia 12 na mwaka huu
tutaendelea kupunguza kodi ya mapato kwa wafanyakazi,” alisema Rais Kikwete.
Ukiwa
mwaka wake wa mwisho madarakani, hakuwa na uhakika wa kufikia kiwango
hicho kutoka kodi ya mshahara kuwa tarakimu mbili hadi moja.
“Ndiyo
tuko kwenye mchakato wa bajeti sijui kama kweli tutafikia kwenye
asilimia tisa ninayosema lakini naamini hatutakuwa mbali sana kama
hatutafikia,”alisema na kuongeza:
“Kama tutabakisha patakuwa ni padogo
kiasi ambacho naamini kwamba huyo Rais anayefutia atamalizia halafu
sifa atapata yeye… kwamba yule mzee tulipiga risala hasikii. Amejitahidi
kupunguza, lakini hakufikia pale, wewe umefika asilimia tisa mwaka huo
huo.”
Pia
Rais huyo mstaafu aligusia suala la kima cha chini cha mshahara kwa
wafanyakazi wa sekta binafsi na kusema kuwa hupangwa na bodi za
mishahara ya sekta hizo, ambazo zinaundwa na waziri wa kazi.
“Hadi
kufikia mwaka 2011, tulikuwa na bodi za mishahara za kisekta 12, ambazo
zimeweza kufanya majadiliano na waajiri na waajiriwa katika sekta
binafsi,” alisema Kikwete.
0 comments :
Post a Comment