Wadakwa Wakisafirisha kilo 500 za Mirungi kwa Kutumia Gari Dogo

Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia wakazi wawili wa Mtaa wa Nyegezi, Wilaya ya Nyamagana, Mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ramadhani Ng’anzi alisema jana kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Mei 17, saa nane mchana katika Kijiji cha Mulyaza wilayani Butiama wakiwa na kilo 500 za dawa hizo zimehifadhiwa kwenye vifurushi 15 yenye uzito wa zaidi ya nusu tani.

Alisema watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha dawa hizo kwa kutumia gari aina ya Toyota Carina lililokuwa likiendeshwa na mmoja wao wakitokea Sirari, Wilaya ya Tarime wakielekea Mwanza.

Hata hivyo, aliwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kusaidia kuwakamata watu wanaokiuka sheria na taratibu za nchi.

Baadhi ya wakazi wa mjini hapa walisema udhibiti wa dawa za kulevya ni jukumu la kila Mtanzania kwa sababu madhara yake husababisha athari katika jamii inayozunguka eneo husika.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment