Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) imeendelea jana kwa mchezo mmoja kati ya Manchester United iliyyokuwa mgeni kwa West Ham mchezo uliokuwa ukiamua nafasi ya Manchester United kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mchezo huo ulimalizika kwa West Ham kuibuka na ushindi wa goli 3-2, magoli yakifungwa na Diafra Sakho dk. 10, Michail Antonio dk. 76 na Winston Reid dk. 81 huku magoli ya Manchester United yakifungwa na Anthony Martial katika dakika ya 51 na 72.
Bada ya matokeo hayo Manchester United wamebaki nafasi ya tano na alama 63 ikiwa nyumba ya Manchester City iliyo nafasi ya nne na alama 65 huku wote wakibakiza mchezo mmoja, kwa maana hiyo ili Manchester United ifuzu Ligi ya Mabingwa inahitaji kupata ushindi katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Bournemouth na Manchester City ipoteze mchezo wake.