Kama wote wamefariki basi hatahitaji idhini.
Kuna wakati katika mazingira fulani mahakama inaweza kutoa idhini kwa binti kuolewa akiwa na miaka 14 lakini si chini ya hapo ikiwa ataonekana kwa mfano ana mimba.
Pia mwanaume anaweza kuruhusiwa na mahakama kuoa akiwa na umri wa miaka chini ya 18 lakini lakini si chini ya 16 kama ataonyesha kuelewa jukumu lake kama mtu mzima.
Lakini hii ni pale ambapo kuna tatizo kama la kumpa msichana mimba ndipo mahakama inaweza
ikatoa idhini.
Hii inathibitishwa katika ombi la kuoa la Shabiri A. M Virji (1971) HCD no.407 la Mahakama Kuu ya Tanzania, mwombaji alikuwa na miaka 16 lakini
alimpa mimba binti wa miaka 18.
Mahakama katika kuchunguza ombi la mvulana la kuoa ilitoa kibali kwa sababu wote wawili walipendana sana na wazazi wao hawakuwa na kipingamizi cha wao kuoana.
(f) Kusiwe na ndoa inayoendelea Kama mwanamke ana ndoa inayoendelea na inatambulika kisheria haruhusiwi kufunga ndoa nyingine (polyandry).
Kadhalika kama mwanamme ana ndoa ya mke mmoja au kama ni mwislamu ana wake wanne tayari hataruhusiwa kufunga tena ndoa.
(g) Kusiwe na kipingamizi
Kama ndoa imezuiwa na Mahakama au halmashauri ya usuluhishi kutokana na uwezo zilizopewa na ndoa ikaendelea kufungwa kabla ya wenye kupeleka kipingamizi hawajasikilizwa au Mahakama imeshaamua ndoa hiyo isifungwe basi ndoa hiyo itakuwa ni batili.
(h) Mfungishaji ndoa kutokuwa na mamlaka Kama wanaofunga ndoa wanajua wazi kuwa anayewafungisha ndoa hana mamlaka hayo na kwa makusudu wakakubali awafungishe ndoa basi ndoa hiyo itakuwa ni batili.
Mfungishaji ndoa ili kuwa na mamlaka anapaswa kusajiliwa na Msajili Mkuu wa Ndoa na kupewa leseni ya kufungisha ndoa.
(i) Kutokuwepo kwa wafunga ndoa Kama ndoa imefungwa bila ya wafunga ndoa wote kuwepo basi ndoa hiyo haitambukuliwa kisheria.
Hata hivyo sheria inaruhusu ndoa kufungwa ikiwa mmoja wa wafunga ndoa hayupo, kama mfunga ndoa ambaye hayupo amewakilishwa na mtu ambaye alikuwepo wakati mfunga ndoa hayupo, alipotoa ridhaa yake ya kuoa au kuolewa.
(j) Mashahidi wa ndoa
Ili ndoa itambulike kisheria ni lazima ishuhudiwe na mashahidi wasiopungua wawili ambao wanaruhusiwa
kisheria yaani umri wao usipungue miaka 18 na wafahamu kinachosemwa na kutendeka wakati wa kufunga ndoa.
(k) Kuwa katika eda
Eda ni kipindi cha kukaa ndani kinachotolewa kwa mwanamke wa kiislamu aliyeachika katika ndoa au aliyefiwa na mumewe, ili taratibu fulani za kidini
Itaendelea…


Blogger Comment
Facebook Comment