Baada ya kutolewa katika mashindano ya Uefa Euro 2016 na kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson kuchukua uamuzi wa kujiuzulu kuifundisha timu hiyo, nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Wayne Rooney amejitokeza na kutoa maoni yake kuhusu kocha ambaye wa kuifundisha timu hiyo.
Rooney alisema kuwa ni jambo sahihi nafasi hiyo akipatiwa kocha Mwingereza ambaye ana uwezo mkubwa wa kufundisha soka na atakayeweza kuisaidia timu ya taifa hilo kufanikiwa kisoka.
“Anatakiwa kuwa na uwezo wa ziada ili aifanye kazi yake vizuri, awe Mwingereza au siyo lakini tusubiri na kuona, nadhani anatakiwa kuwa mtu ambaye anautaifa na ambaye ni mtu bora,
“Nadhani itakuwa sahihi kama akiwa Mwingereza, ni sahihi awe Mwingereza lakini ambaye atakuwa ni sahihi kwa kazi hiyo,” alisema Rooney.