Mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), amepandishwa kizimbani
baada ya kujisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es
Salaam, kujibu tuhuma za kuchapisha chapisho la uchochezi lenye kichwa
cha habari' Machafuko yaja Zanzibar'.
Lissu
alifika mahakamani hapo jana saa tano asubuhi, kwa ajili ya kuitikia
wito wa kumtaka kwenda kujibu tuhuma za uchochezi zinazomkabili baada ya
washitakiwa wenzake wawili akiwemo Mhariri wa Mawio ambalo lilifungiwa
kwa muda usiojulikana, Simon Mkina kusomewa mashitaka.
Mbunge
huyo na washitakiwa wenzake Mkina na mchapishaji wa Kampuni ya Jamana,
Ismail Mehboob, walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas
Simba.
Upande
wa jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Paul Kadushi kwa
kushirikiana na Salim Msemo, ulidai mahakamani hapo kuna washitakiwa
Lissu, Mkina na Mehboob na mshitakiwa Jabir Idrisa bado hawajampata na
wamepata taarifa anaumwa.
Kadushi
aliomba kumsomea mashitaka Lissu, ambapo alimsomea mashitaka matatu ya
kula njama kuchapisha chapisho la uchochezi, kuchapisha taarifa yya
uchochezi na kosa la tano ambalo ni mbadala wa kosa la pili la kutishia.
Wakili
huyo alidai Lissu na wenzake kati ya Januari 12 hadi 14, mwaka huu, Dar
es Salaam, walikula njama ya kuchapisha chapisho la uchochezi katika
gazeti la Mawio lenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja
Zanzibar’.
Pia
Lissu na wenzake walidaiwa Januari 14, mwaka huu, Dar es Salaam, kwa
nia ya kuleta chuki na uchochezi kati ya wananchi na mamlaka halali ya
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, walichapisha chapisho hilo lenye
uchochezi.
Aidha,
Lissu alidaiwa siku hiyo kinyume cha sheria na bila ya mamlaka
waliwatishia na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar wasiweze kuingia
kwenye marudio ya Uchaguzi Mkuu.
Lissu
alikana mashitaka hayo, ambapo Hakimu Simba alisema Juni 14, mwaka huu,
shauri lilipokuja kwa mara ya kwanza upande wa utetezi ulileta
pingamizi juu ya uhalali wa mashitaka wakiomba yafutwe.Kesi hiyo
itatajwa Julai 14, mwaka huu



Blogger Comment
Facebook Comment