Safari ya msimu wa tano wa mashindano ya Maisha Plus imeanza rasmi kwa kuanza na usaili uliofanyika katika hotel ya NAF Beach iliyoko Mtwara. Washiriki kutoka mikoa ya jirani nao pia walijitokeza. "Maisha Plus kwangu ni ndoto ya muda mrefu sana, niliposikia mnakuja Mtwara nikasema piga ua lazima nishiriki" Anasema Ismail Likando aliyesafiri kutoka Lindi.
Ni asubuhi tulivu katika fukwe za bahari ya hindi kusini mwa Tanzania ambapo vijana wengi wamejitokeza kufanya usaili wa mashindano ya Maisha Plus East Africa 2016. Wapo wanaoonekana kujiamini na wengine wamejawa uoga. "Ni siku niliyoisubiri kwa hamu sana" anasema Faustine Komba miongoni mwa washiriki kutoka Mtwara.
Muhitimu wa shahada ya kilimo William Mbaga alibanwa kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ikiwemo faida za kilimo cha 'greenhouse' pamoja na namna ambavyo maziwa ya mtindi yanapatikana. William alijieleza kwa ujasiri.
William Mbaga akiondoka baada ya kufanya usaili.Washiriki wenye fani na ujuzi mbalimbali walijitokeza wakiwemo madereva bodaboda, mafundi, waigizaji, waimbaji, wasusi n.k
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.Kwa picha zaidi BOFYA HAPA(P.T)
Blogger Comment
Facebook Comment