KAPTENI
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi la Tanzania (JWTZ), Henrick Mahenge (34)
mkazi wa Mliman City, Dar es Salaam, juzi alipandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashitaka ya kujaribu kumuua askari
wa usalama barabarani.
Akisoma
mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan, Wakili wa
Serikali, Grace Mwanga alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Julai
12, mwaka huu maeneo ya Mnazi Mmoja wilayani Ilala. Mwanga alidai kuwa
mshitakiwa alijaribu kumuua askari wa usalama barabarani WP 5177
Clesensia Makanyaga.
Mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo.
Hata
hivyo, Mwanga alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na
kwamba hali ya mgonjwa haijulikani hivyo aliomba mahakama izuie dhamana
hadi watakapopata uhakika kuhusu hali ya mgonjwa.
Mshitakiwa
alipopewa nafasi ya kuelezea kilichotokea, alidai hakutishia kuua na
kwamba yeye ndiye alifanyiwa fujo na kuchaniwa nguo zake na kwamba
alimuona mshitakiwa baada ya tukio na kwamba hakupata taarifa kuwa
mlalamikaji yupo hospitali.
Hakimu
Hassan alisema kuwa dhamana ipo wazi kwa wadhamini wawili kutoka
taasisi zinazotambulika na kuwataka wakaguliwe kwanza kujiridhisha.
Alisema
pia mshitakiwa arudishwa rumande hadi Julai 19 mwaka huu
watakapojiridhisha na wadhamini pamoja na kujua hali ya mlalamikaji.
Blogger Comment
Facebook Comment