Safari
ya kibarua cha kocha mpya wa Manchester United, Jose Mourinho imeanza
kwa mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya wa 2016/2017 dhidi ya
Wigan Athletic kwa ushindi wa goli mbili kwa bila.
Magoli
ya Man United katika mchezo huo yalifungwa Will Keane katika dakika ya
49 baada ya kipindi cha kwanza kushindwa kufungana na goli la pili
likifungwa na Andreas Pereira katika dakika ya 58.
Mchezo
huo pia uliwajumuisha wachezaji wapya wa Man United, kiungo Henrikh
Mkhitaryan na beki Eric Bailly huku beki Luke Shaw ambaye aliumia
mwanzoni kwa msimu wa 2015/2016 akirudi dimbani.
Blogger Comment
Facebook Comment