Majambazi Yateka Kijiji Kwa Masaa Matatu Mkoani Kagera



MAJAMBAZI wanne wamevamia kijiji cha Benaco kilichopo katika Wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwa muda wa saa tatu ambapo wamefanikiwa kupora Sh milioni 2.4 na simu ambazo hazikujulikana idadi yake kwa mfanyabiashara mmoja wa huduma ya M-Pesa.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kagera ambaye pia ni ofisa upelelezi wa polisi mkoa huo, Abel Mtagwa, alisema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana ambapo majambazi hao walikuwa na silaha moja ya kivita aina ya SMG.

Alisema kuwa wakati majambazi wakijiandaa kuondoka eneo hilo walimpiga risasi mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Gankabo Wilayani Kibondo mkoani Kigoma aliyetambuliwa kwa jina la Nelson Simon (15) na kumjeruhi mguu wake wa kulia. Mwanafunzi huo amelazwa katika hospitali teule ya Murgwanza iliyopo wilayani humo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment