Waziri Nape Nnauye ametoa tamko hilo huku akizitaja tuhuma mbalimbali zikiwemo:  Uchochezi, Uongo na Upotoshaji ambapo hazizingatii kanuni za taaluma ya uandishi wa habari.
 Amri hiyo ya kulifungia gazeti la mseto imetokana na tangazo la Serikali namba 242 la tarehe 10/8/2016 kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 sura 229 kifungu cha 25(1)
Aidha, Waziri Nape amesema gazeti hilo linaandika habari na taarifa za uongo ambazo zina nia ya kupotosha jamii ikiwa ni pamoja na kutumia nyaraka za serikali ambazo zimegushiwa ili kuwachafua viongozi wa serikali na seerikali yao.
                                          Na Hashim Ibrahim- UDSM-SJMC                                                               
Mseto_front_1470283189
Moja ya toleo la gazeti la MSETO ambalo Waziri wa Habari, Nape amelitaja kukiuka misingi ya taalum ya Habari. Waziri amesema kuwa toleo hilo (Pichani) Wamiliki na Mwandishi wa Gazeti walishindwa kutoa vielelezo vya Habari waliochapisha licha ya kuchapisha nyaraka za kweli huku habari ikiwa ni ya uongo.
DSC_5080
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akitangaza maamuzi hayo ya kulifungia rasmi kuanzia leo  Agosti 11.2016  kwa miezi 33, Gazeti la MSETO la kila Wiki linalochapishwa hapa nchini. Mkutano huo umefanyika katika chumba cha mikutano cha Wizarani hapo.
“juzi wameandika habari ambayo kwakweli ilikua na nia ya kumchafua Mh.Raisi na serikali kwa ujumla,Hivi karibuni gazeti hilo hilo toleo namba 480 la tarehe 4 Agosti hadi 10 Agosti lilichapisha na kusambaza makala na barua ya kugushi kutoka katika Shirika la Taifa la madini STAMICO yenye kicha cha habari kisemacho WAZIRI AMCHAFUA JPM, AMUHUSISHA NA RUSHWA YA UCHAGUZI MKUU, NI NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA MAWASILIANO ” amesema nape
DSC_5091
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye katika tukio hilo.
“Kwa mujibu wa vyombo vya uchunguzi vya serikali, imebainika kuwa  nyaraka hiyo imegushiwa na wahariri au waliohusika kugushi na walipotakiwa kuleta uthibitisho wa nyaraka waliyoitumia katika gazeti lao walishindwa kuleta uthibitisho huo”.
DSC_5103
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akitangaza maamuzi hayo ya kulifungia rasmi kuanzia leo  Agosti 11.2016  kwa miezi 33, Gazeti la MSETO la kila Wiki.
“Ninatoa wito kwa wamiliki , wahariri, waandishi na watangazaji wa habari kuzingatia sheria kanuni na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari ambayo vikizingatiwa hatutakuwa na mgogoro wowote,”
“Aidha serikali inasisitiza kwamba tunaheshimu uhuru wa vyombo vya habari unaozingatia maadili, weledi na sheria za nchi na serikali itashirikiana na wale ambao wapo tayari kufatata sharia hizo.” alimalizia Waziri Nape.
DSC_5106
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akifafanua jambo
DSC_5112
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati wa kutangza tamko hilo.
DSC_5113
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akitangaza maamuzi hayo ya kulifungia rasmi kuanzia leo  Agosti 11.2016 kwa miezi 33, Gazeti la MSETO la kila Wiki. (Picha zote na Andrew Chale).