Baraza la Michezo Tanzania (BMT) lipo katika mchakato wa kutaka kujiridhisha juu ya tukio la Rais wa TFF Jamal Malinzi kuamua kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama chama cha soka mkoa wa Kagera wakati akiwa bado ni kiongozi wa juu wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF).
Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja amethibitisha taarifa hiyo: “Tunaangalia katiba zao zinasemaje kwanza, kwasababu sasahivi bado tunaangalia historia kwakua viongozi waliopita hawakufanya hivi. Sijaiona katiba ya chama alichogombea kule (Kagera) nikijiridhisha nitatoa majibu.”
Kama BMT itajiridhisha kwamba Malinzi amegombea kwa mujibu wakanuni na taratibu, basi atakuwa salama, lakini kama atakuwa nje ya katiba basi BMT itajua nini cha kufanya.
0 comments :
Post a Comment