Mwaka mmoja baada ya kuondoka Manchester United, mshambualiaji wa zamani klabu hiyo, Robin Van Persie anataraji kurejea katika uwanja wa Old Trafford aliouchezea kwa misimu mitatu 2013-2015.
Hatua hiiyo inakuja baada ya klabu anayochezea sasa ya Fenerbahçe kupagwa kundi moja na Manchester United katika hatua ya makundi ya Ligi ya Vilabu Barani Ulaya (UEFA Europa League).
Fenerbahçe na Manchester United zote zipo kundi A zikiwa na timu zingine ambazo ni Feyenoord na Zorya, michezo ambayo inataraji kuchezwa Septemba, 15.
Kabla ya kuondoka Man United, Van Persie aliichezea klabu hiyo michezo 86 na kufunga magoli 46.
0 comments :
Post a Comment