Mwanamuziki maarufu wa Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel anayefahamika kwa jina la kisanii Kiss Daniel aliyetamba hasa kwa kibao chake cha ‘Woju’ kwenye anga za muziki,  ametua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa Tamasha la Monte Carlo Classic lililoandaliwa na Str8up Vibes wakishirikiana na DeJurist Global kwa udhamini wa Benki ya Barclays Tanzania.
Mwimbaji huyo wa Nigeria aliyejizolea mashabiki wengi tangu alipoachia kibao chake cha ‘Woju’, ataongoza uzinduzi wa Tamasha hilo Jumamosi hii jijini Dar es Salaam katika Mgahawa wa Akemi uliopo kwenye jengo la Jubilee Towers, Mtaa wa Ohio.
Akizungumza mapema leo kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Str8up Vibes, Sniper Mantana alithibitisha mbele ya waandishi kwamba maandalizi ya Tamasha hilo yamekamilika na kuwasihi Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kujumuika na msanii huyo maarufu.
1b
(Kutoka kulia) Mkurugenzi wa Stra8up Vibes, Sniper Mantana ambao ni waandaaji wa Tamasha la “Monte Carlo Classic’ akizungumza na waandishi wa habari (hawapo) pichani wakati wa kumtambulisha Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama ‘Kiss Daniel’ atakayepamba uzinduzi wa Tamasha hilo litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es salaam. Pamoja nae ni Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera, Msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel, mbia wa Tamasha hilo kutoka Malaysia DeJurist Global na Meneja wa Msanii huyoLouiza Williams.
Aliongeza kwamba kabla ya Tamasha hilo tiketi zitauzwa kwa shilingi 25,000 na itakapo timu usiku tiketi zitauzwa kwa shilingi 35,000.
Alisema Tamasha la “Monte Carlo Classic” limelenga kubadilishana uzoefu baina ya Watanzania hususani kwenye sekta ya burudani.
“Kwenye miji kama vile;-Monte Carlo, New York, Los Angeles (L.A), Paris watu maarufu hushiriki kwa kupamba matukio kama haya. Hii ni sawa na ambavyo sisi tumelenga kuliimarisha tamasha la Monte-Carlo Classic jijini Dar es Salaam, ambapo kwa usiku mmoja kila mtu anakuwa mtu wa hadhi ya juu, huku akisherehekea na mtu maarufu aliyeteuliwa na kwenye eneo lenye hadhi ambalo limeandaliwa na waandaaji,” alisema.
Kwa mujibu wa Meneja Masoko wa Benki ya Bacrays Tanzania, Joe Bendera, alisema benki hiyo imekuwa ikidhamini ligi kubwa ya soka ulimwenguni jambo ambalo limeifanya kuisogeza karibu na jamii. Tunayo furaha kuwa sehemu ya uzinduzi wa Tamasha kama hili kubwa jambo ambalo litatuwezesha kukutana na wageni waalikwa mbalimbali na wateja wetu.
Tamasha la Monte Carlo Classic DeJurist Global
Mmoja wa washiriki katika uandaaji wa Tamasha la Monte Carlo Classic DeJurist Globalkutoka Malaysia akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kumtambulisha msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel ambaye yupo nchini kwa ajili ya kupamba uzinduzi wa Tamasha hilo litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es salaam. Pamoja na kulia ni Msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel, Meneja masoko wa benki ya Barclays, Joe Bendera na Mkurugenzi wa Sta8up Vibes, waandaji wa Tamasha Sniper Montana. Benki ya Barclays ni wadhamini rasmi wa Tamasha hilo ambalo limezinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
“Tukio hili linatupa fursa ya kutoa elimu kuhusu matumizi ya kadi zetu na kuhamasisha matumizi yake sehemu mbalimbali kwenye mashine za mauzo maeneo mbalimbali nchini. Mwezi uliopita Benki ya Barclays ilitunukiwa cheti cha ubora cha Mtoaji wa Kadi Bora za Visa nchini Tanzania.
Pia katika kubeba fedha taslimu kuna kiwango maalumu hivyo tutapata fursa ya kuwahamasisha wateja wetu kutumia kadi zetu za Debit na Cretid kwenye tukio hili,” alisema
Kwa upande wake msanii huyo alisema alishtuka alipopata mwaliko kutoka kwa Str8up Vibes na kumchague yeye kuwa mgeni rasmi kwenye tukio hilo, na kwa mara ya kwanza kuja hapa nchini kama msanii.
 “Nimefuarahi sana kualikwa kwenye tukio la Monte Carlo Classic hapa jijini Dar es Salaam, ninashukuru kwa nafasi hii na ninapenda kuwashukuru waandaji kwa kutambua umuhimu wangu.”
Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera
Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera akipiga Selfie na Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama Kiss Daniel mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari katika hafla ya kumtambulisha msanii huyo atakayepamba uzinduzi wa Tamasha la “Monte Carlo Classic” litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es salaam. Benki ya Barclays ni wadhamini rasmi wa Tamasha hilo ambalo limezinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
5
Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama Kiss Daniel akionesha albamu yake kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mkutano wa kutambulisha uwepo wake katika Tamasha linalozinduliwa jijini Dar es salaam siku ya kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es salaam.
6d
Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama Kiss Daniel (katikati) akifurahia jambo na Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera (kulia) sambamba na Mkurugenzi wa Stra8up Vibes Sniper Mantana (kushoto) mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari wa kumtambulisha msanii huyo atakayepamba uzinduzi wa Tamasha jipya nchini la “Monte Carlo Classic” litakalofanyika kesho kwenye ukumbi wa Akemi uliopo Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam.
7
Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama Kiss Daniel (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari wa kumtambulisha msanii huyo atakayepamba uzinduzi wa Tamasha jipya nchini la “Monte Carlo Classic” litakalofanyika kesho kwenye ukumbi wa Akemi uliopo Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam.