Askofu mmoja wa kanisa la Grantham, Diocese ya Lincoln nchini Uingereza amejitokeza hadharani na kukiri kuwa amekuwa akishiriki mapenzi ya jinsia moja.
Askofu huyo anayefahamika kwa jina la Nicholas Chamberlain amekuwa askofu wa kwanza nchini Uingereza kujitangaza kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja (ushoga).
Askofu Chamberlain aliwekwa mwaka jana wakfu na Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Justin Welby katika Diocese ya Lincoln na Askofu Mkuu, Welby alisema kuwa anafahamu kama askofu, Chamberlain anashiriki vitendo vya ushoga.
“Anajihusisha na vitendo hivyo kwa muda mrefu,” alisema Askofu Mkuu, Welby na kuongeza.
“Kuchaguliwa kwake kuwa askofu wa Grantham ni kwasababu ya uwezo wake na aliitwa kuja kuhudumu katika kanisa la Diocese ya Lincoln”
Kwa upande wake Askofu Chamberlain alisema anatii miongozo ya kanisa hiyo kwani inaruhusu watu wa jinsia moja kushiriki vitendo vya ngono.
0 comments :
Post a Comment