Mwanasiasa mkongwe,
Philemon Ndesamburo amedai hatua ya Rais John Magufuli kuteua
wakurugenzi wa halmashauri nje ya mfumo wa Serikali, umewavunja moyo
watumishi wengine.
Ndesamburo
ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Mjini (2000-2015), alisema mfumo
huo ulikuwa ukiwajenga watumishi kutoka madaraja ya chini hadi
uandamizi, hao ndiyo walikuwa wakiteuliwa.
Julai
7, Rais Magufuli aliteua wakurugenzi 185 kati yao 65 ndiyo walioteuliwa
kutoka orodha ya zamani ya wa kurugenzi na 120 ni wapya.
Kati
ya hao wapya, wapo walioteuliwa miongoni mwa makada wa CCM walioshindwa
kura za maoni ndani ya chama hicho 2015 na wengine wakitoka nje ya
mfumo wa utumishi wa umma.
Ndesamburo
alidai hatua ya Rais kuteua makada wa CCM nje ya mfumo kushika wadhifa
huo, utaziyumbisha halmashauri nyingi kwani wengi hawajui namna ya
kushughulikia madokezo.
“Kwenye
baadhi ya halmashauri hao ambao walionekana hawawezi kuwa promoted
(kuteuliwa), ndiyo wanaowafundisha wakurugenzi wapya. Hapa kidogo Rais
wetu alichemka,” alidai Ndesamburo.
Akizungumza
katika mahojiano maalumu jana, Ndesamburo alidai nafasi
za uteuzi kama za wakuu wa mikoa na wilaya, Rais angeweza kuteua makada
wa CCM lakini siyo ukurugenzi.
CHANZO :Swahiba news



0 comments :
Post a Comment