WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imezifuta
shule za awali, msingi na sekondari nchini ambazo hazijasajiliwa zaidi
ya 40 kuanzia Julai mwaka jana.
Awali kuanzia Julai hadi Desemba
mwaka jana, waligundua kuwepo kwa shule 35 zisizosajiliwa na kuzifuta,
jambo lililofanya kutangaza shule zote ambazo hazijasajiliwa
kujisalimisha ili kusajiliwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Usajili wa Shule
katika wizara hiyo, Khadija Mcheka alisema Mei mwaka huu baada kuzipa
miezi
miwili shule ambazo hazijasajiliwa kufanya hivyo, walizifungia
shule nyingine 12.
Alitaja shule zilizofungiwa kwa kuendesha
shughuli zake bila usajili kuwa ni shule za awali na msingi za Must Lead
ya mkoa wa Pwani, na za mkoa wa Dar es Salaam ni Brainstorm, Pax,
Lassana, Grace, Rose Land, Julius Raymod, St Thomas, Mary Mother of
Mercy, Noble Sinkonde, Immaculate Heart of Mary, St Columba, Corner
stone, Dancraig, Mwalimu Edward Kalunga, Edson Mwidunda, Gisela,
Kingstar, St Columba awali, Bilal Muslim, Thado, Hocet , Elishadai,
Lawrance Citizen, Comrade, Dar Elite Preparatory na Golden Hill Academy
na Hekima.
Nyingine ni Pwani Islamic, St Kizito na Rwazi
Encysloped za Kagera, Dancraig na Qunu za Pwani, Hellen’s ya Njombe,
Joseph ya Arusha, Samandito na Maguzu za Geita. Alizitaja shule za
Sekondari zilizofungiwa kwa sababu hiyo kuwa ni Hananasif, Elu, Hocet,
Safina za Dar es Salaam na Namnyaki ya Iringa.
Aidha, Shule ya Fountain Gate ya jijini Dar es Salaam imefungiwa kwa kuendesha bweni bila kibali.



0 comments :
Post a Comment