Ujumbe wa Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ukiongozwa na
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Vincent Mashinji umewasili katika Wizara
ya Mambo ya Nje ya Ujerumani, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya
siku 7 katika nchini hiyo.
Pia imewataja wengine waliopo kwenye msafara huo kuwa ni, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA, Zanzibar Zeudi Mvano Abdillahi, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Ruth Mollel, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ilala Anatropia Theonest.
Katika ziara hiyo ya kikazi iliyoanza Septemba 18, ujumbe huo mbali ya kufika Wizara ya Mambo ya Nje ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, kwa ajili ya mazungumzo, pia utafika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya nchi hiyo.
Aidha utakutana na kufanya mazungumzo na Wabunge wa Bunge la Shirikisho la Nchi ya Ujerumani na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini humo, kujadiliana na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali, hususan kiuchumi na kisiasa.



0 comments :
Post a Comment