Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuanzia sasa mtu yeyote mwenye shida ya
kuonana naye itabidi amfuate Dodoma na kwamba atarudi Dar es Salaam
pindi akiitwa na Mheshimiwa Rais au Makamu wa Rais.
Ametoa
kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Septemba 30, 2016) wakati akizungumza na
viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa Dodoma waliofika kumpokea mara
baada ya kuwasili mjini hapa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake
aliyoitoa Julai 25 kuwa atahamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu.
“Tukio
hili la kuhamia Dodoma si la mzaha, hakuna siasa na wala si jaribio.
Tumeshatekeleza. Kama kuna waliokuwa wanafikiria kwamba halitekelezeki
watambue kwamba tayari tumeshafika. Na kuanzia sasa atakayetaka huduma
ya Waziri Mkuu aende Dodoma.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiagana na watuimishi wa makazi
ya Waziri Mkuu ya Dar es salaam kabla ya kuondoka kuelekea Dodoma jana
Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu amesema Dodoma si ndogo kama baadhi ya watu wanavyodai na kwamba
huduma zilizopo zinatosha kukidhi mahitaji ya sasa. “Mkakati uliopo wa
kupanua huduma za tiba, maji, umeme na masoko utawezesha watumishi wote
kuishi bila bugudha yoyote.
“Awamu
ya kwanza inaanzia Septemba hadi Februari mwakani. Mimi nimeshatangulia
na wanaofuata ni mawaziri na manaibu wao wote, Makatibu Wakuu na Naibu
Makatibu Wakuu wote. Natambua kwamba wote wana nyumba za kuishi na kama
wapo ambao hawana hawazidi asilimia tano na nyumba zipo
Amewataka
watumishi wote wa Serikali watambue kwamba safari imeshaanza na kila
mmoja ajipange, na akarudia wito wa Mheshimiwa Rais kwamba atakayegoma
kuhamia Dodoma atakuwa amejifukuza kazi.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia akiwapungia wananchi
wa Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba
30, 2016.
Waziri
Mkuu amewataka watendaji wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma
(CDA) wasifanye kazi kwa mazoea, bali wabadilike na kwa kuwa amehamia
Dodoma ameahidi kuafuatilia kwa karibu zaidi.
Mapema
akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nchi (OWM SUBKAV), Jenista
Mhagama amesema kilichofanyika leo ni uthibitisho kuwa yale ambayo
Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi sasa hivi imeanza kuyatekeleza.
“Tuliahidi
kukusanya kodi, tuliahidi elimu bure, tuliahidi kupambana na mafisadi,
tuliahidi kuondoa watumishi hewa, tuliahidi kuifufua ATCL na kununua
ndege mpya na yote tumetekeleza,” amesema.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa
Manispaa ya Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma
Septemba 30, 2016.
Naye
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. George Simbachawene amesema
uamuzi wa kuhamia Dodoma ni uthibitisho kuwa viongozi wetu kweli
wamedhamiria kutekeleza ahadi ya Baba wa Taifa ya kuhamishia makao makuu
ya nchi hapa Dodoma.
“Dodoma
imeanza kuchangamka na hii ni fursa tosha kwa mkoa wetu kubadilika.
Tushirikiane na CDA kuijenga Dodoma mpya. Kitendo cha Mheshimiwa Waziri
Mkuu kuingia Dodoma leo hii maana yake ni kwamba Serikali iko rasmi
Dodoma,” amesema.
Hafla
hiyo ilihudhuriwa na Manaibu Waziri Anthony Mavunde na Dk. Ashatu
Kijaji, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais
(Utumishi), Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo, wazee wa mkoa huo, viongozi wa
dini, viongozi wa taasisi zilizoko mkoani na baadhi ya wananchi.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye makazi yake mjini Dodoma Septemba 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea ufunguo ikiwa ni ishara ya
kukaribishwa Dodoma na Meya wa Manispaa ya Dodoma Jafar Mwanyemba katika
mapokezi yaliyofanyika kwenye makazi yake , Mlimwa Septemba 30, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Dodoma
baada ya kukaribishwa kimira na wazee hao Septemba 30, 2016.
Mke
wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizawadiwa vazi la kimila na wanawake wa
Dodoma ikiwa ni ishara ya kumkaribisha karika Manispaa hiyo, Septemba
30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
0 comments :
Post a Comment