Tangu
kuanza kwa msimu wa 2016/2017 wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) wadau
mbalimbali wa soka duniani wamekuwa wakimzungumzia nahodha wa Manchester
United, Wayne Rooney kuwa ameshuka kiwango.
Baada
ya maneno kuwa mengi ambayo yanazungumzia kiwango chake, Rooney
amezungumzia jambo hilo na kueleza kuwa yeye anafanya kitu ambacho
anaagizwa kufanya na sio kuwasikiliza watu wengine.
“Namsikiliza
kocha wangu na wachezaji wenzangu, watu ambao wapo karibu yangu na
sisikilizi mambo ambayo watu wengi wanasema sababu mengi wanayozungumzia
ni maneno machafu,
“Ninatakiwa
kuwa makini, kujituma, na kweli nimeshalifanya hilo katika maisha yangu
ya soka. Ninajituma sana na kujitahidi kuonyesha uwezo wangu kwa timu,”
alisema Rooney.
Aidha
Rooney amezungumzia matokeo ambayo timu yake imekuwa ikiyapata kwa siku
za karibuni na kusema kuwa hicho ni kipindi cha mpito na anaamini
watarejea katika kiwango bora.
“Tumekuwa
na wiki mbaya, siku nane mbaya ambazo tulipoteza michezo mitatu, ni
muhimu sasa kujipanga vizuri kwa ajili ya hilo na kuja na njia mbadala,”
alisema Rooney.


0 comments :
Post a Comment