Usome hapa ujumbe wa Lowassa kwa watanzania baada ya leo kuwasili Kagera


Ijumaa ya Septemba, 23 aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CHADEMA, Edward Lowassa amewasili mkoani Kagera kwa ajili ya kuwajulia hali waathirika wa tetemeko la ardhi ambalo lilitokea Septemba, 10 mwaka huu.
Baada ya kuona hali ilivyo sasa kwa baadhi ya wakazi wa mkoa huo kupoteza ndugu zao, nyumba na mali zao kuharibika, Lowassa ametumia ukurasa wake wa Twitter kufikisha ujumbe kwa jamii ya watanzania sehemu yoyote walipo duniani kote.
Ujumbe wa kwanza Lowassa aliandika “Poleni ndugu zangu Wa Kagera na mlioathirika na tetemeko, Tupeane nguvu ili tuvuke katika kipindi hiki kigumu pamoja”
Na ujumbe wa pili Lowassa aliandika “Nawasihi watanzania wenzangu tuendelee kujitolea kuwasaidia wahanga kama ilivyo desturi ya umoja wa kitaifa tulionao”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment