Usiku wa November 22 2016
zilichezwa mechi nane za UEFA Champions Leagua hatua ya Makundi,
miongoni mwa michezo iliyochezwa usiku wa November 22 ni pamoja na
mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Sporting CP klabu iliyomlea
Cristiano Ronaldo.

Mchezo huo ambao ulichezwa katika dimba
la Jose Alvande , mashabiki wa Ureno walipata fursa ya kumuona nyota wao
Cristiano Ronaldo akihusika kutengeneza goli la kwanza la Real Madrid
katika ushindi wa goli 2-1, kipigo hicho kimewafanya Sporting kusubiri
mchezo wa kukamilisha ratiba.

Sporting CP ikiwa nyumbani katika uwanja
wao wenye uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya elfu 50000, wamekubali
kipigo cha goli 2-1 magoli yakifungwa na Raphael Varane dakika ya 29 na
Karim Benzema aliyetumia vyema krosi ya Sergio Ramos dakika ya 87, huku
Andrien Silva akipachika goli la kufutia machozi kwa Sporting dakika ya
80.



0 comments :
Post a Comment