Leo
October 7, 2016 Nkupamah media imepata taarifa ya majibu ya
madaktari juu ya uchunguzi wa Macho ya kijana Said maaarufu kama Baba D
ambaye alipata mkasa wa kushambuliwa na mtu anayefahamika kwa jina la
Scorpion, kisha kutobolewa macho yote mawili hali iliyopelekea kutoona.
Jitida
zilizofanywa na Serikali ya mkoa wa Dar es salaam zikiongozwa na mkuu wa
mkoa Paul Makonda ili kuweza kumsaidia kijana huyo zilifanikiwa
kumfikisha katika Hospitali ya Muhimbili ambako alifanyiwa uchunguzi wa
kina ili kujua kama kuna uwezekano wowote wa kumrejeshea uwezo wa kuona.
Majibu ya
madaktari yametolewa leo na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda na kuzua
hali ya huzuni kwa Said na familia yake wakiwemo mama mzazi, mama mkwe
na mkewe baada ya ripoti ya Madaktari kuonesha kwamba hakuna uwezekano
wa aina yoyote ambao unaweza kumfanya kijana huyo akaja kuona tena.
Mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam Paul Mkaonda amesema Serikali ya Mkoa itampa Said
kiasi cha Shilingi Milioni 10 kwaajili ya kuanzisha biashara
itakayomsaidia yeye na familia yake, pia amesema kutakua na gari ambayo
itakua ikimsaidia kwenye shughuli zake pamoja na kumsomesha kwenye shule
za watu wenye ulemavu wa macho.


0 comments :
Post a Comment