MUUGUZI HOSPITAL YA WILAYA YA CHUNYA MBEYA ATIWA MBARONI KWA KUDAIWA KUSABISHA KIFO CHA MTOTO MCHANGA


Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa akizungumza na watumishi wa hospital ya Wilaya ya Chunya kufuatia tukio la mama mjamzito kifanyiwa vitendo vya unyanyasaji na mmoja wa watoa huduma hospitalini hapo hali iliyopelekea mtoto kupoteza maisha .

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa akimfariji Maria Solomoni ambaye alipoteza mtoto wake   kwa uzembe wa muuguzi katika katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
Patricia Kisoti Muuguzi anayetuhumiwa kufanya uzembe uliosababisha Mama mjamzito kujifungua na mtoto wake kupoteza maisha katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
Mkuu wa Wilaya Chunya Rehema Madusa akiwa na majonzi baada ya kumsikia mama aliyepoteza mtoto wake mara baada ya kujifungua kutokana na uzembe wa muuguzi katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
Baadhi ya watumishi wa hospital ya Wilaya ya Chunya katika Mkutano na Mkuu wa Wilya y chunya mara baada ya kutokea tukio la mama mjamzito aliyepoteza mtoto wakati akijifungua kutokana na uzembe wa mmoja wa wauguzi hospitalini hapo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Chunya,
Sasita Shabani akizungumza kuhusiana na tukio hilo la kufanyiwa ukatili kwa mama mjamzito na mmoja wa wauguzi .
Wananchi na wanaopata huduma za afya katika Hospita ya Wilaya Chunya wakionesha nyuso za majonzi mara baada ya mmoja wa wananchi kufanyiwa vitendo vya kikatili.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chunya,
Sophia Kumbuli akisisitiza jambo kuhusiana na tukio hilo.
Wananchi
na wanaopata huduma za afya katika Hospita ya Wilaya Chunya wakionesha
nyuso za majonzi mara baada ya mmoja wa wananchi kufanyiwa vitendo vya
kikatili.

Jeshi la Polisi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya linamshikilia muuguzi
wa afya katika  hospitali ya Wilaya ya
Chunya, Patricia Kisoti, kwa kutokana na uzembe uliopekekea mama mjamzito
kujifungua mtoto akiwa amekufa.
 
Akizungumzia tukio la kukamatwa kwa muuguzi huyo Mwenyekiti wa
kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Chunya
Rehema Madusa amesema kitendo kilicho fanywa na muuguzi huyo nichakinyama
na kimetia aibu sekta ya afya.
 
Amesema September 4, mwaka huu katika hospitali ya Wilaya ya Chunya,
mjamzito huyo akiwa  ameongozana na mwenzake walifika kituoni hapo usiku,
wakihitaji huduma ya haraka kutokana na hali ya mgonjwa kuwa mbaya.
 
Amesema licha ya mama huyo kufika akiwa katika hali mbaya
alijitahidi kujieleza ili apate huduma kwa waaguzi waliokuwa zamu akiwemo
mtuhumiwa huyo Patricia Kisoti ambaye ndiye aliyetakiwa kumhudumia mgonjwa huyo
lakini alishindwa kutoa ushirikiano badala yake alitoa majibu ya kejeli na
kushindwa msaada wowote.
 
Amesema kama mama huyo angemshughulikiwa kwa haraka ikiwa na
muuguzi huyo kutoa taarifa kwa ngazi za juu baada ya kuona tatizo hilo
haliwezi, basi mtoto huyo angekuwa hai.
 
Aidha, Mkuu huyo alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chunya,
Sophia Kumbuli kuhakikisha anachukua hatua za kinidhamu kwa wahusika wote.
 
Amesem kifo cha kichanga hicho, kwa asilimia kubwa  kilitokana na uzembe wa muuguzi huyo kutokana
na maalezo yaliyotelewa mgonjwa huyo.
 
Akizungumzia sakata hilo, Maria Solomoni, amesema  siku hiyo,
yeye akiwa ameongozana na mwenzake aliyemtambulisha kuwa alikuwa ni wifi yake,
walifika katika kituo hicho cha afya majira ya usiku, huku akiwa ameshikwa na
uchungu, ambapo waligonga mlango wa chumba cha nesi ambao kwa muda huo ulikuwa
umefungwa.
.
Maria, aliendelea kufafanua kuwa aliendelea kuteseka na mates
ohayo mpka majira ya saa kumi namoja alifajili ndipo alipoona wanaume wawili
wakimuhangaikia na kumuingiza katika chumba cha upasuaji na kufanyiwa
oparesheni.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Chunya,
Sasita Shabani, alikiri kutokea kwa tukio hilo kituoni hapo na kwamba katika
uchunguzi wao wa awali umebaini kwamba katika tukio lililomkuta Maria Solomoni,
ndani yake kulikuwa na uzembe.
Mwisho.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment