Ligi
Kuu ya Uingereza (EPL) imeendelea kwa michezo mbalimbali kupigwa leo
Jumapili ya Septemba, 2 na mmoja wa michezo huo ukiwa ni mchezo wa
Tottenham Hotspur iliyokuwa mwenyeji wa Manchester City katika dimba la
White Hart Lane.
Mchezo
huo umemalizika kwa Tottenham kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa
bila, magoli ya Tottenham yakifungwa na Aleksandar Kolarov kwa kujifunga
dakika ya tisa na Dele Alli dakika ya 37 ya mchezo huo.
Ushindi
wa Tottenham umemaliza utemi wa Manchester City kwani katika michezo
sita iliyokuwa imecheza kabla ya leo ilikuwa imeshinda michezo yote, na
huu unakuwa mchezo wa kwanza kwa Manchester City kufungwa tangu awasili
kocha Pep Guardiola.


0 comments :
Post a Comment