Siku ya Jumapili November
13,2016 timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itashuka dimbani kucheza
na wenyeji Zimbabwe mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa kwenye
uwanja wa Taifa wa Harare mjini Harare.
Mchezo huo utachezwa majira ya
saa tisa alasiri kwa saa za Zimbabwe wakati Tanzania itakuwa saa kumi
jioni kwa saa za Afrika Mashariki na utakaoneshwa na kituo cha
Televisioni ya Taifa ya Zimbabwe (ZBC) na hapa nyumbani wataungana na
kituo cha Televisioni cha Azam TV.
Wakiwa chini ya kocha Mkuu
Boniface Mkwasa kikosi chote kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja
wa Harare na tayari kwa vita hiyo ya Kesho na ushindi wa kesho utakuwa
na faida ya kuipandisha Tanzania katika viwango vya FIFA.
Mchezaji wa timu ya Tanzania
Mbwana Samatta ambaye pia anachezea timu ya Genk ya Ubelgiji akiwa na
mchezaji mwenzake Thomas Ulimwengu wakijiandaa kwa mazoezi mjini Harare
nchini Zimbabwe tayari kwa mchezo wao na timu ya Taifa ya Zimbabwe
jumapili.
wachezaji wa timu ya Taifa Taifa Stars wakijiandaa kwa mazoezi.
Mchezaji Thomas Ulimwengu akibeba majiya kunywa kwenye toroli kwa ajili kunywa wakati wa mazoezi ya timu hiyo.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa taifa Stars Boniface Mkwasa akijadiliana jambo na makocha wenzake.
Mazoezi yakiendelea.


0 comments :
Post a Comment