UGANDA ‘THE CRANES’ YAIBUGIZA KIJIKO KIMOJA CONGO,KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018.


uganda-cranes

Na.Alex Mathias.

Nyota wa Uganda ‘The Cranes’Farouk Miya,anayecheza katika klabu ya Stadard Liege inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji ameipa pointi tatu timu yake ya Taifa ya Uganda baada ya kuwalaza Congo goli 1-0 mchezo wa kutafuta nafasi ya kufuzu kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Ilikuwa dakika ya 18 Miya aliwanyanyua mashabiki wa Uganda waliokuwa wamefurika katika kutazama mechi hiyo licha ya kupata goli hilo waganda walipata upinzani mkubwa toka kwa wageni hadi mapumziko wenyeji walikuwa mbele kwa goli hilo moja.

Kipindi kilianza kwa timu zote kushambuliana huku vijana wa Micho wakicheza mpira wa kushambulia na kukaba na kuwanyima uhuru Wacongo hao hadi kipyenga kinamalizika Uganda wamezoa pointi tatu muhimu.

Na kwa matokeo hayo Uganda wamefikisha pointi 4 na kuongoza kundi huku wakiwa wanasubiri mchezo wa kesho wa kundi hilo utakaowakutanisha wababe wa soka timu za Ghana watakaocheza na Misri ambao wana pointi 3 na Ghana wakiwa na pointi moja ambayo waliipata kwa sare na Uganda.

Uganda itaikaribisha tena Misri Februari 28,mwakani wakati Congo watakuwa nyumbani kwao kucheza na black Stars Ghana.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment