Jela Miaka 30 Kwa Kumnajisi Binti Wa Miaka 9

Mahakama  ya Wilaya ya Ilala, imemhukumu Shabani Huseni (29), kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kunajisi mtoto wa miaka tisa.

Akisoma hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi Catherine Kihoja alisema upande wa mashitaka ulipeleka mashahidi watano ambao wameweza kuthibitisha mashitaka bila kuacha shaka yoyote.

“Kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapa umeweza kuthibitisha mashitaka hivyo, mshitakiwa ninamtia hatiani kama alivyoshitakiwa,’’alisema Hakimu Kioja.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo Wakili wa Serikali, Neema Moshi, aliomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mujibu wa sheria kwa kuwa mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho ameathirika kisaikolojia na kupata madhara kiafya kutokana na kutokwa na harufu mbaya sehemu zake za siri.

Aidha, mshitakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kile alichodai kwamba hana ndugu, ombi ambalo lilitupiliwa mbali.

Inadaiwa kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo tarehe isiyofahamika Julai mwaka jana eneo la Kipunguni B, Moshi Baa wilayani Ilala ambapo alimbaka mtoto wa miaka tisa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment