Magufuli Akutana Na Mke Wa Mwanzilishi Wa Taifa La Sudani Kusin

Mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  Alhamisi ya tarehe 08 Desemba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini Rebecca Nyandeng Garang de Mabior.

Baaada ya mazungumzo hayo,Mke huyo wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini Rebecca Mabior amesema yeye pamoja na ujumbe wake wamelazimika kufika nchini Tanzania kuonana na Rais Dkt Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuia ya afrika ya Mashariki kwa lengo la kumfahamisha hali halisi ya nchi ya Sudan ya Kusini.

Amemuomba Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake wajumuia ya Afrika ya Mashariki kulisaidia Taifa la Sudan ya Kusini kutafuta suluhisho la mgogoro unaolikabili taifa hilo na kurejesha amani.

"Tumefarijika kuwa hapa katika ikulu ya Tanzania na tuko hapa kumsihi Rais Dkt Magufuli kama Mwenyekiti wa jumuia ya Afrika ya Mashariki akishirikiana na viongozi wenzake wa jumuia hiyo kuona namna gani wanaweza kutusaidia ili Taifa la Sudani ya Kusini liwe Taifa lenye amani,hivyo hapa tunawakilisha vilio vya watu wa nchi yetu na kikubwa tunachokitaka ni Amani katika nchi yetu na hiki ndio kilio chetu"

Rais Magufuli kwa upande wake amewasihi viongozi na wananchi wa Sudan ya Kusini kutafuta njia muafaka ya kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani na ili kuepuka machafuko yanayosababisha mateso kwa wananchi wa Taifa hilo.

"Mama Rebecca hata mimi binafsi naumizwa na kile kinachoendelea katika nchi ya Sudani ya Kusini hivyo,ningezisihi pande zote zinazotofautiana kumaliza tofauti zao kwa amani kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa la Sudani ya Kusini"

Emmanuel Buhohela
Kaimu Mwandishi wa habari Msaidizi wa Rais.
Dar es Salaam
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment