Dereva wa Zitto Kabwe aongea baada ya kukamatwa na Polisi



Jana January 23 2017 tulisikia taarifa kutoka jeshi la polisi Shinyanga kuhusu kukamatwa kwa gari alilokua analitumia kiongozi wa chama cha ACT WAZALENDO ambae pia ni Mbunge wa Kigoma mjini Zitto kabwe.
Ilidaiwa kwamba sababu ya gari hilo kukamatwa ni kosa la kutokuwa na vibali halali huku Polisi ikimtaka Zitto ajitokeze na leo dereva Patrick Muhidin akiwa Dodoma amepata nafasi ya kueleza ukweli mbele ya kamera ya Ayo TV na kusema…>>>’Tulikuwa kwenye kampeni za uchaguzi baadae baada ya kumaliza mkutano Zitto alikwenda kuonana na viongozi wake
Muda kidogo askari walinifuata wakiwa na gari zao kama tano kisha wakamuulizia kiongozi, baadae tena wakaniambia tuchukue gari nililokuwa naendesha kisha twende kituoni‘ –Patrick Muhidin
Waliniandikisha maelezo na wakataka niwape vibali vya gari na mimi nikafanya hivyo, wakaniambia nikabidhi lile gari na kunitaka niondoke ili mmiliki alifuate‘ –Patrick Muhidin
Vipi kuhusu madai ya kumiliki gari lisilokuwa na vibali halisi? ‘Ukweli gari lina vibali vyote halali na niliwapa siku ileile ya jumamosi na walibaki nayo kuanzi siku hiyo hadi jana walivyonikabidhi‘ –Patrick Muhidin
Unaweza kuendelea kumsikiliza dereva akisimulia yote kwenye hii video hapa chini…
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment