Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Joseph
Magufuli, kesho tarehe 25 /01/2017 anatarajiwa kuzindua Awamu ya Kwanza
ya Miundombinu na Utoaji wa Huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka (Bus Rapid
Transit - BRT) katika Kituo Kikuu cha Mabasi kilichopo Kariakoo eneo la
Gerezani jijini Dar es salam.
Uzunduzi
huo utahudhuriwa na Rais wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, Bw.
Makhtar Diop na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia wa nchi za Tanzania,
Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird.
Awamu
ya Kwanza ya mradi wa ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka
(BRT) yenye urefu wa kilometa 20.9 unaojumuisha barabara ya Kimara –
Kivukoni, Magomeni - Morocco na Fire – Kariakoo ulikamilika Desemba
2015.
Aidha,
utoaji wa huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka ulianza tarehe 10 Mei, 2016.
Kwa sasa huduma ya mabasi katika kipindi cha mpito inatolewa katika
njia nane, vituo vikuu vitano, vituo vidogo 28 na karakana moja kwa
kutumia mabasi 140 yanayojumuisha mabasi makubwa 39 yenye uwezo wa
kubeba abiria 160 kila moja na mabasi madogo 101 yenye uwezo wa kubeba
abiria 60 kila moja.
Mradi
wa ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) umepangwa
kutekelezwa kwa awamu sita kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari
katika Jiji la Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Eng. Joseph M. Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI)
0 comments :
Post a Comment