Iringa mjini
Mji wa Iringa ukionekana kwa mbali
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (mwenye suti nyeusi) akitatua
moja ya mgogoro wa ardhi mkoani Iringa.
………………
Na Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na ziara zake za
utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambapo jumatano hii tarehe 25
Januari 2017 atawapatia wakazi wa kijiji cha Kinywang’anga Iringa
vijijini.
Katika ziara hii Mhe. Lukuvi
atakutana na wananchi hao waliopimiwa maeneo yao ya viwanja na mashamba
ambao kwasasa hati zao za umiliki wa ardhi hizo zimeishaandaliwa na
ziko tayari kukabidhiwa kwao.
Ziara hii ni katika utekelezaji wa
Programu ya Kitaifa ya kupima na kumilikisha ardhi na kuzuia migogoro
ya ardhi wenye lengo la kufanyika kwa nchi nzima. Utekelezaji huo
utahusisha kuhakiki mipaka ya Mitaa na Vijiji pamoja na maeneo mengine
yote nchini na kupima kila kipande cha ardhi kwa lengo la kumilikisha
ardhi hiyo kwa wananchi, taasisi na Kampuni.
Sambamba na hilo, Matangazo ya
Serikali yanayotambulisha mipaka ya mikoa, Wilaya, Hifadhi za Taifa na
vijiji yatafanyiwa marekebisho baada ya mipaka yote nchini kuhakikiwa na
kukamilika.
Aidha mpango huu unalenga
kuwaunganisha wadau wa sekta ya ardhi katika kupanga, kupima, na
kumilikisha ardhi nchini na kuweka kumbukumbu za vipande vya ardhi ili
kuongeza thamani ya ardhi na kuondoa migogoro ya ardhi kwa ajili ya
maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Serikali ya awamu ya tano imeweka
adhma ya kumaliza migogoro ya ardhi iliyopo sasa na kuzuia kasi ongezeko
la migogoro ya ardhi ndani ya miaka mitano kwa kuandaa mpango kabambe
wa matumizi na usimamizi wa ardhi kwa kuharakisha na kurahisisha
upatikanaji wa hati za umiliki wa viwanja na mashamba
0 comments :
Post a Comment