Mchezaji
wa timu ya Kagera Sugar, David Abdalah Burhan ambaye pia amewahi
kuchezea klabu mbalimbali za bongo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo
katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
amethibitisha kutokea kifi hicho na kutuma salamu zake za pole kwa
familia pamoja na klabu ya Kagera Sugar na kwa wote ambao wameguswa na
kifo cha mchezaji huyo.
"Nimepokea
kwa masikitiko taarifa za kifo cha David Abdalah Burhan mchezaji wa
Kagera Sugar. Amefariki usiku wa kuamkia leo.Apumzike kwa amani"
Marehemu
David Burhan ameshawahidakia Mbeya City na Majimaji, ikumbukwe kuwa
Burhan ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Pan African ya Dar es
Salaam, Abdallah Buruhan.
0 comments :
Post a Comment