Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 32 kujeruhiwa vibaya baada ya basi
la Vitu Laini linalofanya safari zake kutoka vijiji vya Kilolo kwenda
Iringa Mjini kugongana na lori la mbao karibu likiwa limekaribia kufika
Iringa Mjini.
Akizungumza na Nkupamah media, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP
Peter Kakamba amethibitisha kutokea kwa ajli hiyo na kueleza kuwa
majeruhi wote wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Iringa.
“Ni kweli ajali imetokea leo asubuhi nje kigogo ya Mji wa Iringa, basi
ndilo limegonga lori kwa nyuma na kusababisha kifo cha mtu mmoja
aliyeaga dunia palepale na kusababisha majeruhi 32.
“Majeruhi wote tumewapeleka katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa ambako
wanaendelea kupatiwa matibabu mpaka sasa. Alisema Kamanda Kakamba.
Kuhusu chanzo cha ajali hiyo haijafahamika kama ni matatizo ya gari au
mwendoksasi wa dereva hivyo Kamanda Kakamba amesema watatoa taarifa
rasmi baabdaye kuhusu tukio hilo.
0 comments :
Post a Comment