Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtambua Benjamin Samweli
Sita (pichani) kuwa meya wa Kinondoni. Hukumu hiyo imetolewa leo baada
ya mahakama kutupilia mbali hoja za upande wa pili Ukawa waliofungua
kesi kupinga matokeo ya ushindi huo.
Itakumbukwa kuwa, siku ya uchaguzi huo, polisi waliwakamata baadhi ya
viongozi na wajumbe wa UKAWA sambamba na ongezeko la wajumbe batili
upande wa CCM.
CHADEMA na Ukawa walifungua kesi katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupinga ushindi Meya wa Manispaa ya
Kinondoni, Benjamin Sitta huku walalamikaji wakiwa ni Mustapha Muro
(aliyekuwa mgombea Meya Manispaa ya Kinondoni) na Jumanne Amir Mbunju
(aliyekuwa mgombea Naibu Meya wa Manispaa hiyo) wote wakiwakilisha na
Wakili wa CHADEMA, John Malya.
Kesi iliyofunguliwa dhidi ya Afisa Utawala wa Manispaa ya Kinondoni,
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Samweli Sita
(aliyetangazwa kuwa Meya) na Manyama Mangaru (aliyetangazwa kuwa Naibu
Meya).
0 comments :
Post a Comment