Mkuu
wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt.Leonald Masalle, kwa niaba ya
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, akifungua Kongamano la Maaskofu wa Jumuiya ya
Makanisa ya Kiinjilisti Ulimwenguni Agape WUEMA kutoka nchi za Afrika
Mashariki na Kati, linalofanyika kwa siku mbili (leo na kesho) Jijini
Mwanza.
Kongamano
hilo limelenga kujadili na kuazimia mgawanyo wa ujenzi wa miradi ya
jumuiya hiyo katika nchi sita za Afrika Mashariki na Kati (Tanzania,
Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Kongo) ambayo ni pamoja na Makanisa,
Shule na Hospitali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa mataifa husika.
Aliyesimama kulia ni Askofu Mkuu wa Agape WUEMA barani Afrika, Mande Wilson, akizungumza kwenye kongamano hilo.
Askofu Mkuu wa Agape WUEMA Tanzania, Martin Gwilla, akizungumza kwenye kongamano hilo
Maaskofu mbalimbali wa jumuiya ya Agape WUEMA kutoka mataifa ya Afrika Mashariki na Kati
Binagi Media Group
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema serikali itaendelea
kushirikiana na taasisi za kidini katika kufanikisha miradi mbalimbali
ya maendeleo inayotekelezwa na taasisi hizo.
Hayo
yamebainishwa katika risala yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya
Ilemela, Dkt.Leonald Masalle kwenye ufunguzi wa kongamano la Maaskofu wa
Jumuiya ya Makanisa ya Kiinjilisti Ulimwenguni AGAPE WUEMA kutoka nchi
za Afrika Mashariki na Kati, linalofanyika Jijini Mwanza.
Amesema
serikali inaunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na jumuiya hiyo
katika kufanikisha utekelezaji wa miradi yake nchini ikiwemo ujenzi wa
makanisa, shule pamoja na hospitali.
Askofu
Mkuu wa Jumuiya hiyo, Martin Gwila, ameishukuru serikali kwa ushirikiano
wake ikiwemo kuruhusu ujenzi wa miradi iliyokusudiwa ambapo ameomba
ushirikiano huo kuwa endelevu kwani miradi hiyo itaongeza chachu ya
maendeleo katika jamii.
Askofu
Mkuu wa Jumuiya ya AGAPE WUEMA barani Afrika, Mande Wilsoni,
amebainisha kwamba kongamano hilo lililowakutanisha zaidi ya Maaskofu
170 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati limelenga kuhakikisha ugawaji
na utekelezaji wa miradi iliyokusudiwa unaanza mapema mwaka huu.
0 comments :
Post a Comment