Kundi
la kigaidi linalojiita ‘Islamic State of Iraq and Syria’ (ISIS) kwa
mara ya kwanza limetajwa kufanya mashambulizi ya mlengo wa kigaidi
Jerusalem nchini Israel.
Waziri
Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema kuwa shambulizi la kutumia
roli lililowaua watu wanne na kujeruhi wengine 17 lilifanywa na kijana
wa Palestina aliyetumwa na kundi la ISIS.
Israel
ilifanya kikao cha dharura cha kabineti ya usalama ambacho ingawa
hakikutoa vielelezo kuhusu mtu huyo, kilimtaja kuwa mfuasi wa ISIS.
“Tunajua
kumekuwa na mlolongo wa mashambulizi ya kigaidi. Kuna uhakika kuwa
kunaweza kuwa na muungano kati yao [ISIS], kutoka Ufaransa hadi Berlin,
na sasa Jerusalem,” alisema Netanyahu.
Mshambuliaji
huyo aliyetambulika kwa jina la Fadi Qunbar mwenye umri wa miaka 28,
raia wa Palestina alitumia lori kubwa kuwagonga watu hao lakini alipigwa
risasi na kuuawa papohapo baada ya kutekeleza tukio hilo.
Watu kadhaa wamekamatwa kutokana na tukio hilo wakiwemo majirani zake na wana familia wake watano.
0 comments :
Post a Comment