Rais
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein amewataka
wananchi wa Zanzibar kufanya kazi na kutodanganyika kuwa ataondolewa
madarakani na mtu yeyote.
Akizungumza
jana visiwani humo mbele ya wananchi, Dk. Shein alieleza kuwa hakuna
mtu au taasisi yoyote itakayotawala Zanzibar wakati yeye bado yuko
madarakani.
“Hakuna
atakayeweza kuingilia masuala ya Zanzibar, hakuna atakeyongoza Serikali
hii wakati mimi bado ni ko madarakani. Msidanganywe,” alisema Dk. Shein.
“Hakuna cha Umoja wa Mataifa wala Katibu Mkuu gani atakayekuja kuiongoza Serikali hii wakati mimi niko madarakani,” alisisitiza.
Rais
Shein ameyasema hayo wakati ambapo Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi
(CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amekuwa katika harakati anazoziita
kuishtaki Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Umoja wa Mataifa
akidai kupokonywa ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
CUF
inashiriki uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Dimani, ikiwa ni
miezi takribani tisa tangu chama hicho kisusie uchaguzi wa marudio
uliofanyika mwaka jana baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25 akieleza kuwa ulikubwa
na kasoro nyingi.
0 comments :
Post a Comment