Mtu
mmoja anayejiita Nabii nchini Afrika Kusini amezua taharuki baada ya
picha kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwanywesha
waumini wake kemikali ya kusafishia injini na kusema kuwa ina ladha kama
asali.
Nabii Theo Bongani Maseko wa kanisa la Breath of Christ Ministries lililopo mjini Johannesburg amesema kuwa kemikali hiyo inashambulia virusi ndani ya mwili wa binadamu na kutambua mapepo.
Maseko alisema kuwa unywaji wa kemikali hiyo hauna madhara yoyote kiafya kwani yeye mwenyewe amewahi kunywa.
“Ina ladha kama asali, nimewahi kunywa mara mbili” alisema Maseko.
Aidha,
alisema kuwa waumini wake wote ambao tayari wameshatumia dawa hiyo
hakuna hata mmoja aliyepata matatizo ya kiafya na kwamba wote wamekuja
na ushuhuda wa kuponywa matatizo yao. Alisema kuwa Mungu alimpa wito huo
kabla hata hajazaliwa.
Nabii
huyu si yeye pekee aliyefanya vitu vya kushangaza kwani kuna mwingine
alikuwa akiwapulizia waumini dawa ya kuuwa wadudu na mwingine
akiwanywesha petroli.






0 comments :
Post a Comment