Mshambuliaji wa timu ya Taifa Stars na klabu ya KRC Genk Mbwana Samatta
ameendelea kufumania nyavu kwa mara ya pili Mfululizo katika michezo ya
Ligi Kuu ya Ubelgiji baada ya Genk kuibuka na ushindi wa magoli 3-0
didi ya Kortrijk katika uwanja wao wa Luminus Arena.
Wiki iliyopita Samatta
aliifungia bao muhimu timu yake ugenini dhidi ya As Eupen na usiku wa
kuamkia Leo Samatta amefunga bao lake la Sita msimu huu wa Ligi hiyo.
Katika ushindi wa goli 3-0 mtanzania Mbwana Samatta ameendelea kuwa hodari wa upigaji vichwa, kutokana na kutumia vyema krosi iliyopigwa na Schrijvers dakika
ya 42 na kufunga goli la pili kwa KRC Genk, goli hilo linakuja ikiwa ni
dakika 38 zimepita toka Siebe Schrijvers aifungie Genk goli la kwanza
na Alejandro Pozuelo akafunga goli la tatu dakika ya 68.
Kwa matokeo hayo Genk wamepanda hadi nafasi ya nne ya Msimamo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji wakifikisha jumla ya pointi 34 huku Samatta akifikisha jumla ya magoli Sita na kujiweka katika mazingira mazuri ya kumaliza akiwa na magoli mengi zaidi.
0 comments :
Post a Comment