Shirikisho la soka barani Afrika limechukua hatua ya kuulinda mtandao wake baada ya kubainika ulikuwa umedukuliwa.
Kundi mmoja la Urusi la New World Hackers, linadai lilidukuwa mtandao huo.
Wanachama wa kundi hilo waliiambia
BBC kwamba walifanya hivyo ‘kupinga’ Gabon, mwenyeji wa michuano ya
Kombe la Mataifa ya Afrika.
”Gabon ni nchi ya udikteta,” mwanachama mmoja wa kundi hilo ameiambia BBC Sports.
Shirikisho la soka barani Afrika
(CAF) limeongeza shughuli ya sekunde tano ya kuwachunguza wageni wote
kwenye mtandao wake, ifahamikayo kama Cloudflare, kama njia ya
kukabiliana na shida hiyo.
“CAF imechukua hatua lakini
hatuwezi kusema kwa asilimia 100 kwamba kisa kama hicho hakitatokea
tena,” Junior Binyam, mkurugezi wa maswala ya mawasiliano wa shirikisho
hilo amesema.
”Hata Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) liliwahi kudukuliwa.”
Mtandao wa CAF ulifungwa kwa saa
tano siku ya Jumamosi, na kusababisha viongozi wa bodi hiyo kuchunguza
hitalafu ya kimtandao wakidhani ilikuwa chanzo, kabla ya kubaini tatizo
lilitokana na udukuzi
Mwaka huu michuano ya Kombe la
Mataifa ya Afrika imepingwa na raia kadhaa wa Gabon ambao wametumia
nafasi hiyo kuelezea malalamiko yao ya kisiasa.
Maafisa wa Gabon wamesema watu
watatu waliuawa kutokana na makabiliano makali ya kupinga matokeo ya
uchaguzi uliofanyika mwaka jana.
Upinzani ukiongozwa na mwenyekiti wa zamani wa tume ya Umoja wa Afrika Jean Ping umesema idadi ya waliofariki ilikuwa juu.
Miezi iliyofuata upinzani
uliwataka raia kususia michuano ya soka iliyoanza rasmi tarehe 14
Januari na inatarajiwa kukamilika Februari 5 .
Siku ya Jumapili New World
Hackers, pia walidai kudukua mtandao wa kampuni ya mafuta ya Total,
ambayo ilitangaza udhamini mkubwa wa mamilioni ya dola kwa CAF mwaka
jana.
BBC imejaribu kuwasiliana na kampuni hiyo ya Total lakini hawajasema lolote.
Gabon imekuwa timu ya kwanza kati
ya 23 zilizoadhimisha kombe la afrika kubaduliwa nje katika hatua ya
makundi walipotoka sare na Cameroon.
0 comments :
Post a Comment