Mabingwa watetezi wa kombe la
mataifa ya Afrika timu ya taifa ya Ivory Coast rasmi imevuliwa ubingwa
wa mataifa ya Afrika, baada ya kuruhusu kufungwa goli 1-0 na timu ya
taifa ya Morocco katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi C.
Ivory Coast ambao walikuwa Kundi C
na timu za Morocco, Togo na DR Congo, wamejikuta wakifungwa goli 1-0 na
kushindwa kusawazisha, Ivory Coast wameondolewa katika michuano hiyo
kwa kumaliza nafasi ya tatu na kama wangepata ushindi leo dhidi ya
Morocco wangefuzu kucheza robo fainali.
Kocha wa Morocco Herve Renard
ambaye kawavua Ubingwa Ivory Coast, ndio kocha aliyewapata taji hilo
Ivory Coast mwaka 2015 akiwa anaifundisha timu hiyo, Rachid Alioui ndio
alihitimisha safari ya Ivory Coast kwa goli alilofunga dakika ya 64.
0 comments :
Post a Comment