Baada ya kusota kwa miaka kadhaa
timu ya taifa ya Tanzania ‘Stars’kupangwa kwenye makundi magumu hatimaye
CAF imeipa ahueni na kuipanga katika kundi L, kufuzu Fainali za Kombe
la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon pamoja na Uganda, Cape
Verde na Lesotho.
Hili linaweza kuwa kundi rahisi zaidi Taifa Stars, kwani zote
Uganda, Cape Verde na Lesotho ni timu ambazo zipo ndani ya uwezo wake –
kikubwa ni maandalizi ni mshikamano wa Watanzania kama taifa.
Kenya pia itaanzia hatua ya makundi, ikiwa imepangwa Kundi F
pamoja na Ghana, Ethiopia na Serra Leone, wakati Rwanda ipo Kundi H
pamoja na Ivory Coast, Guinea na Afrika ya Kati (CAR).
Mshindi wa kila kundi atafuzu moja kwa moja AFCON
ya 2019, wakati timu nyingine tatu zitakazomaliza nafasi ya pili na
wastani mzuri zaidi ya nyingine zitafuzu kama washindi wa pili bora.
Michuano hiyo itaanzia kwa hatua ya mchujo, Raundi ya Awali
itakayohusisha timu za Comoros, Djibouti, Madagascar, Mauritius, Sao
Tome E Principe na Sudan Kusini.
Timu zitakazofuzu hapo zitaingia moja kwa moja kwenye
makundi A, B na C kukamilisha idadi ya timu nne nne. Kundi Ab lina timu
za Senegal, Equatorial Guinea na Sudan, B kuna wenyeji Cameroon, Morocco
na Malawi na C kuna Mali, Gabon n Burundi.
Cameroon ikiongoza Kundi, mshindi wa pili atafuzu moja kwa moja
na kama itashika nafasi ya tatu au ya nne, mshindi wa kwanza atafuzu
moja kwa moja na mshindi wa pili atawania nafasi tatu za ziada za kufuzu
kama mmoja wa washindi wa pili bora.
Hatua ya mchu itachezwa kati ya Machi 20 na 28 wakati mechi za
kwanza za makundi zitaanza Juni 5 na 13, za pili Machi 19 na 27 2018, za
tatu Septemba 3 na 11, 2018 za nne Oktoba 8 na 16, 2018 na za tano
Novemba 5 na 13, 2018.



0 comments :
Post a Comment