Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), limemwondoa Mwamuzi Hussein Athuman kwenye orodha ya
waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) baada ya kupata alama za chini
ambazo hazimwezeshi kuendelea tena kuchezesha Ligi hiyo.
Mwamuzi Hussein Athuman kutoka
Mkoa wa Katavi alichezesha mchezo namba 150 uliozikutanisha timu za
Majimaji ya Songea na Young Africans ya Dar es Salaam, kwenye Uwanja wa
Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Kadhalika Young Africans imepigwa
faini ya jumla ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kutokana na timu yao
kutoingia vyumbani, na pia kutumia mlango usio rasmi wakati wa kuingia
uwanjani, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14 (13) na (14) ya
Ligi Kuu. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi
Kuu.
Mwamuzi Ngole Mwangole: Mwamuzi
huyo wa kati, Ngole Mwangole wa Mbeya amepewa barua ya onyo kali na
kumtaka aongeze umakini wakati akichezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom
baada ya kubainika kukataa bao lililoonekana kutokuwa na mushkeli la
Mtibwa Sugar dhidi ya JKT Ruvu katika mechi iliyofanyika Uwanja wa
Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Licha ya kujitetea, lakini kamati
haikuridhika na maelezo yake. Hata hivyo, kwa kuzingatia kuwa Bw.
Mwangole alikuwa Mwamuzi Bora wa msimu uliopita (2015/2016) na hiyo
ndiyo mara yake ya kwanza kuonekana kufanya uamuzi uliokosa umakini
wakati akichezesha, TFF imeamua kumpa onyo.
Mechi namba 141 (Mwadui FC vs
Kagera Sugar). Beki wa Kagera Sugar, Godfrey Taita anapelekwa kwenye
Kamati ya Nidhamu kwa kuwavamia waamuzi baada ya mechi na kuwatolea
lugha chafu na vitisho kabla ya benchi la ufundi la timu yake pamoja na
askari polisi kuingilia kati na kudhibiti kadhia hiyo.
Mechi namba 151 (Mtibwa Sugar vs
Simba). Baada ya mchezo kumalizika mashabiki waliingia uwanjani kwa
wingi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wachezaji, waamuzi na waandishi
wa habari. Pia kamera ya Azam Tv upande wa goli la Kusini iliangushwa
na washabiki hao.
Vilevile sehemu ya kuchezea
(pitch) ya Uwanja wa Jamhuri iko katika hali mbaya ambapo inahitaji
marekebisho makubwa ili iweze kuendelea kutumika kwa ajili ya mechi za
Ligi Kuu ya Vodacom.
TFF imebaini kuwa kitendo cha
washabiki kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho, licha ya kuwa ni
kinyume cha kanuni lakini pia kilichangiwa na askari polisi kutokuwa
makini katika majukumu yao ya kusimamia usalama uwanjani na badala yake
kuelekeza umakini katika kutazama mechi.
Hivyo, Uwanja umesimamishwa
kutumika kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom ili kutoa fursa kwa
wamiliki kufanya marekebisho makubwa kwenye eneo la kuchezea (pitch), na
pia askari polisi kupata maelekezo ya kutosha ya jinsi ya kusimamia
usalama uwanjani badala ya kutazama mechi. Kama marekebisho
hayatafanyika, uwanja huo hautatumika kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya
Vodacom.
LIGI DARAJA LA KWANZA
Mechi namba 34 (Pamba vs Friends
Rangers). Kamishna wa mechi hiyo Mnenge Suluja amepewa Onyo Kali kwa
kutoripoti kitendo cha timu ya Pamba kuhudhuria kikao cha maandalizi ya
mechi (pre match meeting) ikiwa na wawakilishi watatu badala ya wanne.
Kitendo hicho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 35 (Kiluvya United vs
Lipuli). Timu ya Lipuli imepewa Onyo Kali kwa kuhudhuria kikao cha
maandalizi ya mechi (pre match meeting) ikiwa na wawakilishi watatu
badala ya wanne. Kitendo hicho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi
Daraja la Kwanza.
Pia mshabiki wa Kiluvya United,
Bw. Athuman Mzongela anapelekwa Kamati ya Nidhamu kwa kuwavamia waamuzi
na kutaka kuwapiga wakati wa mapumziko. Hata baada ya mchezo aliendelea
kuwatolea lugha chafu waamuzi na Msimamizi wa Kituo.
Mechi namba 36 (African Sports vs
Ashanti United). Daktari wa Ashanti United, Andrea Mbuguni amefungiwa
miezi sita na kupigwa faini ya sh. 200,000 kwa kuondolewa kwenye benchi
baada ya kumtolea lugha chafu Mwamuzi Msaidizi namba moja.
Mechi namba 38 (Lipuli vs
Mshikamano FC). Kocha wa Mshikamano FC, Hamisi Kinonda amefungiwa mechi
tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 baada ya kuondolewa kwenye benchi
kwa kupinga muda wa nyongeza wa dakika tano, na kumtolea lugha ya matusi
Mwamuzi wa Akiba. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 40(11) ya Ligi
Daraja la Kwanza.
Wachezaji wa Mshikamano FC, John
Mbise jezi namba 9, Abdallah Makuburi (5), Ally Mangosongo (12) na kipa
Steven Peter (1) wanapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kumshambulia
Mwamuzi Bryson A. Msuya.
Lakini pia Mwamuzi Bryson A. Msuya
amefungiwa mwaka mmoja kwa kutozingatia sheria ipasavyo wakati akitoa
penalti dhidi ya timu ya Mshikamano FC, na ripoti yake kufanana na ile
ya Kamishna.
Mwamuzi Msaidizi Namba Moja,
Makongo Katuma amefutwa katika orodha ya waamuzi wanaotambuliwa na TFF
kwa kuwapiga vichwa wachezaji wawili wa Mshikamano FC wakati Mwamuzi wa
Kati alipokuwa akishambuliwa na wachezaji wa timu hiyo wakati wakipinga
adhabu ya penalti dhidi yao.
Adhabu hizo ni kwa mujibu wa
Kanuni ya 38(1) na 38(1c) na (1e) za Ligi Daraja la Kwanza kuhusu
Udhibiti wa Waamuzi. Mwamuzi Katuma pia alipata alama za chini ambazo
zisingemruhusu kuendelea kuchezesha Ligi Daraja la Kwanza.
Naye Mwamuzi wa Akiba, Hashim
Mgimba ameondolewa kwenye ratiba kwa kuonyesha muda wa nyongeza (added
time) tofauti na ule alioelekezwa na Mwamuzi. Adhabu dhidi ya Mgimba
imezingatia Kanuni ya 38(1d) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Kamishna wa mechi hiyo Fidelis
Ndenga wa Njombe ameondolewa kwenye ratiba ya makamishna kwa taarifa
yake kufanana na ile ya Mwamuzi. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia
Kanuni ya 39(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Makamishna.
Pia Kamati imetoa mwito kwa vyombo
vya usalama (askari polisi) kutumia nguvu za wastani katika kutuliza
ghasia viwanjani, hasa pale wanapotaka kushughulikia eneo linalohusu
wachezaji.
Uwanja wa Kichangani umeondolewa
kutumika kwa mechi za Ligi, hivyo klabu za Iringa sasa timu zao
zitatumia Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini humo kwa mechi zao la
Ligi. Uwanja huo ulikuwa kwenye matengenezo ambayo tayari yamekamilika.
Mechi namba 39 (Polisi Dar vs
Pamba FC). Klabu ya Pamba imepewa Onyo Kali kwa kutofika kwenye kikao
cha maandalizi ya mechi (pre match meeting). Adhabu hiyo ni kwa mujibu
wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 33 (KMC vs JKT Mlale).
Kocha wa JKT Mlale, Edgar Msabila amefungiwa mechi tatu na kupigwa
faini ya sh. 300,000 baada ya kuondolewa kwenye benchi la ufundi (orderd
off) kwa kutoa lugha chafu. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya
40(11) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 38 (Kimondo FC vs
Njombe Mji). Kocha wa Njombe Mji, Abdul Banyai amefungiwa mechi tatu na
kupigwa faini ya sh. 300,000 kwa kumtolea Mwamuzi lugha ya matusi, na
kulazimisha wachezaji wake wajiangushe ili kupoteza muda.
Mechi namba 40 (Coastal Union vs
Kurugenzi). Wachezaji wawili wa Kurugenzi; Kipa Hamza Mpatula na Optatus
Lupekenya wamefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 kila
mmoja kwa kosa la kupigana wakiwa uwanjani baada ya mechi kumalizika.
Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 37(3) ya Ligi Daraja la Kwanza
kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
Mechi namba 36 (Rhino Rangers vs
Polisi Mara). Klabu ya Rhino Rangers imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa
kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika 20. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni
ya 14(9) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 38 (Mgambo Shooting vs
Rhino Rangers FC). Kocha wa Mgambo, Moka Shabani amefungiwa mechi tatu
na kupigwa faini ya sh. 300,000 kwa kutoa lugha ya matusi kwa Mwamuzi
wakati timu zikielekea vyumbani baada ya kumalizika kipindi cha kwanza.
Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 40(1) ya Ligi Daraja la Kwanza.
LIGI DARAJA LA PILI
Mechi namba 17 (Abajalo vs Burkina
Faso). Klabu ya Burkina Faso imepigwa faini ya sh. 100,000 kwa
kutohudhuria kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting). Adhabu
imezingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za
Mchezo.
Mechi namba 18 (Cosmopolitan vs
Changanyikeni). Klabu ya Changanyikeni FC imepigwa faini ya sh. 200,000
kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani kushangilia ushindi baada ya
filimbi ya mwisho. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi
Daraja la Pili kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mechi namba 19 (Kariakoo vs
Cosmopolitan). Klabu ya Kariakoo imepewa Onyo Kali kwa timu yake
kutokuwa na daktari katika mechi hiyo. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya
14(3).
Mechi namba 16 (Sabasaba vs
Namungo). Klabu ya Sabasaba imepewa Onyo Kali kutokana na washabiki wake
kuwazonga waamuzi wakati wakielekea vyumbani baada ya mechi hiyo
iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kumalizika. Uamuzi huo
umezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Pili.
Mechi namba 17 (Mawezi Market vs
Mkamba Rangers). Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 100,000 kwa
kutohudhuria kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting), na pia
kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika 35. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni
ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.
Mechi namba 19 (Namungo vs Mighty
Elephant). Mighty Elephant imepigwa faini ya sh. 100,000 kutokana na
wachezaji wa akiba na viongozi wake kuingia uwanjani kushangilia bao la
timu yao. Kitendo hicho ni kinyume na Kanuni ya 14(7), na adhabu hiyo ni
kwa mujibu wa Kanuni ya 14(47) ya Ligi Daraja la Pili.
Malalamiko mbalimbali
Malalamiko ya klabu za Mwadui FC
na Polisi Morogoro kuhusu uhalali wa usajili wa mchezaji wa Stand
United, Kheri Mohamed Khalifa na wachezaji wawili wa Njombe Mji kucheza
mechi bila leseni yamepelekwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya
TFF.
Pia maombi ya klabu ya Singida
United kuhusu kubadilishiwa Mwamuzi kwenye mechi yao yamepelekwa Kamati
ya Waamuzi, wakati maombi ya Alliance Schools, Friends Rangers FC, The
Mighty Elephant na Kariakoo FC yanayohusu uendeshaji yanashughulikiwa na
Sekretarieti ya TPLB.
Kuhusu JKT Ruvu
Katika mengineyo, Kamati ilipitia
maombi ya timu ya JKT Ruvu Stars FC kubadilisha uwanja wake wa nyumbani
kutoka Mabatini mkoani Pwani hadi Mkwakwani mkoani Tanga kutokana na
wachezaji wake 12 wa kikosi cha kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi mkoani
Tanga.
Ombi hilo limekubaliwa. Kwa mujibu
wa Kanuni ya 6(6) ya Ligi Kuu, TFF/TPLB zina mamlaka ya mwisho
kuhamisha kituo cha mchezo kwa sababu inazoona zinafaa na kwa wakati
husika.
Kuhusu Mchezaji Venance Ludovic
Pia Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya TFF inatarajiwa kukaa wiki ijayo kusikiliza malalamiko
dhidi ya usajili wa wachezaji mbalimbali akiwemo mchezaji Venance Joseph
Ludovic
0 comments :
Post a Comment