Wakati
mgogoro ndani ya chama cha wananchi CUF ukiwa haujamalizika na suala
hilo kuwa bado lipo mahakamani, leo January 10 2017 Mwenyekiti wa Kamati
ya Uongozi, Julius Mtatiro amekutana na waandishi wa habari na kutoa
kueleza kuwa chama hicho kimeibiwa fedha za ruzuku kiasi cha Tsh Milioni
369.37.
Mtatiro
ameeleza kuwa fedha hizo zilitoroshwa kutoka hazina ya serikali kuu ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania January 05 2017 na kuingizwa kwenye
akaunti yenye jina la The Civic United Front ambapo anasema akaunti hiyo
haikuwahi kuiidhinishwa na Bodi ya wadhamini ya CUF ili ipokee ruzuku
kutoka Serikali Kuu. Unaweza kubonyeza play hapa chini.
0 comments :
Post a Comment