Wabunge wanane waliokuwa wamesimamishwa
kuhudhuria vikao vya Bunge kwa muda na makosa tofauti wanatarajiwa
kurejea kwenye chombo hicho cha kutunga sheria mwisho wa mwezi huu baada
ya kumaliza kutumikia adhabu zao huku baadhi yao wakiahidi kuendeleza
moto wa bajeti.
Wabunge watano kati ya hao waliopigiwa
simu wamesisitiza kwamba wataendelea kubainisha jinsi bajeti iliyotengwa
na Serikali wakati wanasimamishwa ilivyo na changamoto za utekelezwaji
wake.
Mei, 2016 Bunge kupitia Kamati ya Haki,
Maadili na Madaraka ya Bunge ilipitisha azimio la kuwasimamisha
kuhudhuria vikao vya Bunge baadhi ya wabunge wa Kambi ya Upinzani
waliodaiwa kufanya vitendo vya vurugu ndani ya ukumbi na kudharau
mamlaka ya Spika Januari, 27, 2016.
Wabunge hao ni Zitto Kabwe (Kigoma
Mjini), John Heche (Tarime), Halima Mdee (Kawe), Tundu Lissu (Singida
Mashariki), Pauline Gekul (Babati), Godbless Lema (Arusha Mjini) na
Ester Bulaya (Bunda) ambao adhabu yao ilitokana na kitendo chao cha
kupinga msimamo wa Spika kuhusu Bunge kuonyeshwa ‘live’.
0 comments :
Post a Comment